Thursday 25th, February 2021
@
Mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2019 zilizinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan Mkoani Songwe. Mwenge wa uhuru uliwashwa kwa mara yakwanza mwaka 1961 siku ya uhuru wa Tanganyika
nahukimbizwa nchi nzima kila mwaka huku ukibeba ujumbe wa mwenge. Kaulimbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ni
“Maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa”
Mwenge wa Uhuru utaingia mkoa wa Ruvuma tarehe 21/09/2019 na kumaliza mbio zake tarehe 29/09/2019, kwa Halmashauri ya
Mbinga utaingia tarehe 23/09/2019 na kuzindua jumla ya miradi 7. Mwenge utapokelewa katika kata ya Mkako ukitoka Manispaa ya Songea
na mkesha wa Mwenge utakuwa kata ya Mapera.
Wananchi mnaombwa kushiriki katika mbio za mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2019
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2017 Mbinga District Council. All rights reserved. Prepared by IT - Unit