• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima

Sikukuu ya Muungano

Friday 26th, February 2021
@


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wa koloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.


Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:


“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)


Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.


Watanganyika kama ilivyokuwa kwa wananchi wa nchi nyingine za kiafrika, hawakukubaliana hata kidogo na utawala wa kikoloni. Tangu mwanzo waliwapinga na kupigana na wavamizi wa kikoloni, upinzani mkubwa ukionyeshwa na Wasambaa wakiongozwa na Kimweri dhidi ya Wajerumani, Wahehe wakiongozwa na Mkwawa kupigana vichungu na virefu dhidi ya Wajerumani na wakati wa vita vya Maji Maji chini ya uongozi wa Kinjekitile, Mputa na Kibasila.


Kukosekana kwa umoja kati ya wapigania uhuru hawa wa mwanzo na uimara wa majeshi ya wakoloni na silaha bora za moto kulidhoofisha mapambano haya ya uhuru na kusababisha hasara kubwa na kupoteza maisha ya watu.


Kama ilivyokuwa kwenye makoloni mengi ya Kiafrika, hisia za Utaifa ziliendelea kuimarika katika Tanganyika baada ya mwaka 1945. Alama za utaifa zilishaanza kuonekana punde baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kwa kuanzishwa kwa vyama mbalimbali vya Waafrika kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa upande wa Tanganyika, African Association ilianzishwa mwaka 1929 kama kikundi cha mijadala baina ya wasomi na ilipofika mwaka 1948 chama hiki kikawa Tanganyika African Association (TAA). Baada ya vita ya Pili ya Dunia, wanachama wa Tanganyika African Association (TAA) waliendeleza wimbi la utaifa. Mwaka 1953 chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere, TAA ilitambuliwa kama chama cha siasa na kuelekea moja kwa moja kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954 iliyotumika kama chombo cha kisiasa cha watu katika kutoa vilio vyao vya kudai uhuru. Kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954, ulikuwa ndio mwanzo wa mbio za kupigania uhuru. Baada ya miaka saba ya mapambano ya kisiasa, Tanganyika ilikuwa huru chini ya chama cha TANU,kilichoimarishwa na vyama vya wafanyakazi na vya ushirika. 


Kwa upande wa Zanzibar, chimbuko la Jumuiya ya Waafrika ilikuwa ni vilabu vya mpira wa miguu vilivyoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1930. Ilipofika mwaka 1934, Jumuiya ya Waafrika ilianzishwa rasmi na kupewa jina la African Association (AA). Baada ya vita ya pili ya dunia kama ilivyokuwa katika sehemu nyingine za dunia, kulikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, ubaguzi na mgawanyiko baina ya jamii. Kutokana na matatizo hayo ya ubaguzi, kulianzishwa Jumuiya ya Washirazi (Shirazi Association) katika Visiwa vya Unguja na Pemba lengo likiwa ni kudai kupatiwa haki mbalimbali za kijamii na kulinda utambulisho wao. Kuundwa kwa chama cha ZNP (Zanzibar Nationalist Party) mwaka 1957, kulifanya viongozi wa Jumuiya ya Waafrika (African Association) na wale wa Shirazi Association waone umuhimu wa kushirikiana. Waligundua kuwa Serikali ya kikoloni na chama cha ZNP walishirikiana kuendeleza dhuluma dhidi ya Waafrika. Viongozi hao waliona ulazima wa kuungana kuwa kitu kimoja kupigania uhuru. Hivyo, katika kutekeleza azma hiyo, Viongozi wa Jumuiya hizo walikutana na kukubaliana kuunganisha Shirazi Association na African Association mwaka 1957 na kuunda chama kilichoitwa Afro- Shirazi Union ambacho baadae kiliitwa Afro-Shirazi Party .


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - DEREVA MITAMBO II December 28, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI - MSAIDIZI WA HESABU DARAJA II December 24, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA December 18, 2020
  • TANGAZO LA UCHAGUZI 2019 September 10, 2019
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga ahamia na timu yake na Kuanza kazi katika Eneo lake la Utawala

    October 28, 2019
  • Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aagiza Halmashauri ya Wilaya kuhamia kwa muda katika eneo la Kigonsera kabla la tarehe 30/10/2019

    October 22, 2019
  • Mbinga yaweka historia kwa kufanya mnada wa kahawa kwa mara ya kwanza

    September 12, 2019
  • Ziara ya kamati ya fedha, mipango na uchumi yataka miradi kukamilika kwa wakati

    June 01, 2019
  • Tazama zote/kote

Video

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Christine Mndeme aagiza Halmashauri ya Wilaya kuhamiamia Kiamili kabla ya tarehe 30/10/2019
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Iringa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 Mbinga District Council. All rights reserved. Prepared by IT - Unit