Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mh. Cosmas Nyshenye akikabidhiwa hundi na Afisa masoko wa NMB Bwn Baraka Mwabulesi wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa fedha kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu.Jumla ya TSH. MILIONI 198 zimekopeshwa bila riba.Kutoka kushoto ni Kaimu RAS Efrem Simbeye,Mbunge wa Mbinga Mh. Martin Mtonda Msuha, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mh. Cosmas Nyshenye,Mwakilishi wa Benk ya NMB,Baraka Mwabulesi, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Ambrose M. Nchimbi na Mwenyekiti wa CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, imetekeleza agizo la serikali la kuwawezesha Wanawake,Vijana na Walemavu kwa asilimia 100. Halmashauri ya Mbinga ilikisia kukusanya zaidi ya bilioni 1.98 kama mapato ya ndani, na ilitakiwa itoe 10% ya mapato hayo ili kuwawezesha Vijana(4%), Wanawake(4%) na Walemavu(2%). Halmashauri ya Mbinga imeweza kugawa milioni 198 kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Walemavu. Fedha hizo zimegawiwa kwa jumla ya vikundi 48 ambavyo vinajishughulisha na ujasiliamali ndani ya Halmashauri. Kwa mwaka 2017- 2018 Halmashauri iliweza kugawa jumla ya milioni 20 sawa na asilimia 2 kwa mkundi hayo, aidha fedha hizo zilitolewa kwa vikundi hazina riba ila inatakiwa zirejeshwe ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kukopa
ASILI YA FEDHA ZA KUWAWEZESHA VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU
Bunge la Jamhuri ya muungano lilipendekeza kila Halmashauri iwawezeshe vijana na wanawake ili kutatua changamoto ya ajira na kujiongezea kipato kwa wajasiliamali. Serikali ya chama tawala (CCM) katika ilani yake imetaka Halmashauri kutenga 10% yamapato yake nakuwezesha Wanawake,Vijana na Walemavu. Halmashauri ya Mbinga kwa mwaka wa fedha 2019/2020 imeweza kutekeleza ilani ya chama kwa 100% kwa kuwezesha vikundi vya Vijana,Wanawake na Walemavu kwa kuwakopesha milioni 198 bila riba
VIKUNDI VILIVYONUFAIKA NA MIKOPO
Halmashauri ya Wilaya inakanzi data ya vikundi vya wajasiliamali ambapo tathimini yakubaini uhai wa vikundi hivyo, Ofisi ya Maendeleo ya jamii ilipita kwa kila kikundi na kutoa elimu ya namna yakutumia fedha za mikopo. Aidha kila kikundi kilitakiwa kuwa na akaunti benki na kitambulisho cha ujasiliamali.
Orodha ya vikundi na kiwango cha fedha walichokipata ipo katika kiungo hiki(link) MIKOPO 2018-2019.xls.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit