Tarehe 1 Oktoba kila mwaka ni siku ambayo ulimwengu unaadhimishi siku ya wazee, dhumuni kubwa la maadhisho haya ni kuwakumbuka wazee kwa yale walioyafanya kwa kujenga nchi,
kuona changamoto mbali mbali kama ukatili, afya dhidi ya wazee. Halmashauri ya Mbinga imeadhimisha sherehe hizo katika kata ya Matiri ambapo wananchi na wazee mbalimbali walikusanyika na kusherehekea maadhisho hayo.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo:kaimu mkuu wa Wilaya Doc. Patric Banzi, aliisihi jamii kutowatelekeza wazee nakuona jukumu lakuwalea ni letu sote kwani wao pia walitulea na kutufikisha hapa." Lazima tuwaenzi wazee wetu kwani Taifa hili bila wao lisingefika hapa lilipo" alisema mgeni rasmi.Katika maadhimisho hayo ,mgeni rasmi aligawa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee wakata ya Matiri ambapo wazee 426 walipata vitambulisho vyao.
Kauli mbiu ya siku ya wazee mwaka huu ilikuwa " WAZEE NI HAZINA YA TAIFA TUENZI JUHUDI ZA KUTETEA HAKI ZA USTAWI WAO" , Mzee Wiliam Komba wa kijiji cha Kiyaha aliipongeza serikali kwakuwakumbuka na kuwaomba wananchi wote kuona kuwa niwajibu wao kuwajali wazee waliopo.
Kwa picha za sherehe ingia katika ukurasa wa youtube kwenye kiungo hapa chinihttps://youtu.be/7Yf9q5r1CMI
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit