Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepongezwa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.
Hayo yamejiri leo Juni 28, 2021 wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, ambayo imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Mhe. Bedda Hyera ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM Wilaya ya Mbinga, Mhe. Bedda Hyera ambaye pia ameongoza Kamati hiyo amesema wao kama Chama chenye jukumu la kuisimamia Serikali wameridhishwa sana na hali ya miradi yote iliyotembelewa na Kamati hiyo.
"Sisi kama Chama cha Mapinduzi tumeridhika sana na utekelezaji wa miradi, toka tumeanza mpaka tumefika hapa unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga". Amesema Mhe. Hyera
Mwenyekiti huyo amesema ubora wa miradi hiyo ni matokeo ya usimamizi mzuri na hivyo kupelekea kuwa na miradi mizuri yenye ubora, tija kwa jamii na inayoendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo
Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Ndg. Juma Mnwele na menejimenti yake nzima kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo
"Mkurugenzi pamoja na wakuu wako wa Idara, sisi (CCM) hatuna cha ajabu cha kuwapa zaidi ya kuwasemea vizuri, nadhani ukimsemea mtu vizuri mungu anambariki na kumuinua zaidi ya pale alipo". Ameongeza Mwenyekiti huyo.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbinga imetembelea jumla ya miradi saba ya maendeleo, ikiwa ni utaratibu wake wa kila nusu mwaka (miezi 6) wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo huku miradi iliyotembelea kipindi hiki ikiwa ni Shule Teule ya Sekondari ya Wavulana Mbinga (Mbinga Boys) iliyopo Kijiji cha Ndongosi, Ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Ruanda, Kikundi cha Wanawake na Umoja wa Vijana (Ruanda) pamoja na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja Shule ya Msingi Mabuni (Kijiji cha Mabuni).
Miradi mingine iliyotembelewa ni ujenzi wa madarasa mawili, ofisi moja na matundu saba ya vyoo Shule ya Msingi Mtazamagama (Amanimakolo), ujenzi wa ofisi za Halmashauri, kikundi cha vijana cha Chipukizi na mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya, yote ikitelekezwa Kijiji cha Kigonsera
Imeandikwa na
Salum Said,
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Juni 28, 2021
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit