Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Bw. Juma A. Mnwele amewataka watumishi wa Halmashauri
kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu. Hayo aliyasema wakati akihutubia mkutana wa watumishi uliofanyika katika ukumbi wa umati
leo (17/09/2018).
Aidha mkurugenzi alisikiliza kero mbalimbali za watumishi na kuahidi kuzitatua huku akisisitiza uwajibikaji na kupendana katika kazi, " Nafungua milango kwa watumishi wanapokuwa na matatizo au changamoto,waje tujadili tatizo ili waweze kufanya kazi na wakuu wa idara tufanye kazi kwa team work" .
Pia katika mkutano huo afisa Utumishi Wilaya aliwataka watumishi kujali maadili ya kazi na akawasomea majukumu ya watumishi na haki zao.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit