Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ziarani Mkoani Sumbawanga aliagiza kila Halmashauri ambayo inafanya kazi nje ya eneo lake la utawala ihamie kwenye eneo lake la utawala.
Mheshimiwa Mkuuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme aliitisha baraza la dharula lililofanyika tarehe 22/10/2019 nakuagiza Halmashauri ihamie kwa muda katika eneo la Kigonsera kabla ya tarehe 30/10/2019 baada ya kupita katika kata tofauti tofauti.
Wajumbe wa ALAT mkoa wakikagua ofisi mpya za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Kufuatia maagizo hayo Mkurugenzi mtendaji na wataalamu wake tayari wamehamia katika eneo la Kiamili na tayari wameanza kutoa huduma kutokea eneo hilo, aidha kutokanana ufinyu wa ofisi baadhi ya ofisi zimehamia katika jengo la utafiti wa kilimo lililopo katika kata ya Mkako. Wananchi na watumishi wa Mbinga mnajulishwa kuwa Ofisi za Mkurugenzi na timu ya wataalamu wote sasa wanatoa huduma katika eneo lao la utawala .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Mnwele akiwa tayari kuhamisha vifaa vyake na kuhamia katika nyumba mpya huko Kigonsera
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit