Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kikazi Mkoawa Ruvuma na sasa yupo Wilayani Mbinga.
Akiwa Mbinga Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefungua Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, barabara hii inajengwa kwa mkopo wa benki ya Afrika
ambapo itagharimu zaidi ya bilioni 134.
Akihutubia wananchi katika viwanja vya shule Sekondari Makita , alimtaka mkandarasi amalize kazi kwawakati na kumaliza kabla ya mwaka 2020 ili aje aifungue kabla hajamaliza muda wake wa Urais.
. Mkandarasi wa kampuninya CHICO ameahidi kumaliza barabara hiyo ya Mbinga - Mbamba bay kabla ya mwaka 2020 kwakuwa kaambiwa kuwa fedha ipo na yeye amejipanga kuongeza nguvu kazi usiku na mchana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru wa pili kutoka kushoto , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi watatu kutoka kulia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga wapili kutoka kulia, Mwalikishi wa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Chrisianus Ako wa kwanza kulia.
ZIARA YA KUKAGUA SHAMBA LA MAHINDI KITAI
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli , alitembelea gereza lamkilimo Kitai na kufurahishwa na kilimo cha mahindi, awali gereza lakitai lilikuwa likilima ekari zisizo zidi 250 ila katika msimu huu wameweza kulima ekari 650 za mahindi. Aidha amemuagiza kamishna wa Magereza kuwa magereza yakilimo yazalishe zaidi ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa magereza yote na kuokoa fedha ambazo hapo awali serikali ilikuwa ikitoa kuwalisha wafungwa na mahabusu
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit