Afisa Kilimo Mr. Kisima, akipata maelezo toka kwa Wataalam wa Mbegu toka kampuni ya SEED.COM namna mbegu yao ilivyo bora
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni moja kati Halmashauri sita za Mkoa wa Ruvuma, Halmashauri hii inapata wastani wa mvua inayofikia wastani wa 12mm.
kwa mwaka. Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inajumla ya wakazi 345407.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina fursa nyingi za uwekezaji, fursa hizi zinatokana na Hali ya hewa, Uwingi wa watu,Madini na Utalii wa ndani.
MADINI
Halmashauri ya wilaya ya Mbinga imejaliwa kuwa na madini aina nyingi, baadhi ya madini haya ni dhahabu katika kata ya Lukarasi, Makaa ya mawe katika kata ya Ruanda
madini ya vito( gamestone) katika maeneo ya Amani makolo. Halmashauri inawakalibisha wawekezaji ili kuja kuwekeza katika fursa hii ya madini. Leseni za madini zinapatikana katika
ofisi za madini mkoa zilizopo Songea
Picha ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika eneo la Ngaka kata ya Ruanda- Mbinga
VIWANDA
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inazalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara, Wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya kilimo kwa kujenga viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya
mazao tunayozalisha na kuongeza ajira kwa vijana na watanzania kwa ujumla. Kuna viwanda vya kahawa ambavyo vinakoboa kahawa, lakini pia fursa ipo ya kujenga viwanda vingine vya kuchakata kahawa na mazao ya chakula
Picha ya kahawa toka kampuni ya MCCCO.LTD, Kahawa hii imekuwa bora na wananchi inahamisha wananchi kunywa kahawa hii ili kuongeza soko la ndani
KILIMO
Halmashauri ya Mbinga ipo katika nyanda za juu, ambapo mazao ya biashara kama kahawa na korosho yanastawi, wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta ya kilimo.
Mbinga ina jumla ya hekta 150,000 zinazofaa kwa kilimo cha mazao ya biashara. Kwa mwaka Halmashauri ya Mbinga inazalisha zaidi ya tani elfu 20,000 za mazao ya chakula ziada ya chakula
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Kassim Majaliwa akikagua shamba la muwekezaji AVIVI, muwekezaji huyu amekuwa akiandaa miche na kuigawa burena kuhamasisha uzalishaji zaidi wa kahawa katika Halmashauri ya Mbinga
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit