Kata ya matiri ipo umbali wa km 53 toka makao makuu ya wilaya ya Mbinga.Kata ya Matiri ina jumla ya wakazi 14362 ambapo wanaume ni 6755 na wanawake ni 7607, ina vijiji 4(Kihaya,Matiri,Kilindi na Barabara).Kata ya Matiri ina shule za msingi 10 (KILINDI ,KIYAHA, MATIRI, MIKUMI, BARABARA, NGERUKE,NTESUKA na LIMBONI) na sekondari moja, Matiri sekondari inayo milikiwa na serikali. Kuna kituo cha afya,kata ya Matiri ina mradi wa maji ambao umefadhiriwa na serikali jumla.... wanategemea kunufaika na mradi huo.Pia sehemu kubwa ya kata ya Matiri inamawsiliano ya simu za mikonononi kutoka kwa makampuni ya vodacom,tigo na airtel.Kata hii pia ipo katika mpango wa umeme vijijini awamu ya pili.
Pia kuna nyumba za kulala wageni na usafiri wa mabasi wa kwenda Songea na Mbinga.Wakazi wa Matiri ni wakulima wa mahindi na maharage ambapo kwa mwaka 2014 wanategemea kuzalisha tani 45000 za mazao ya chakula. Kata hii pia wanasakosi moja 'MATIRI SACCOS'inayotoa huduma mbali mbali za kibenki
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit