Kata ya Mbuji ipo umbali wa km 31.8 toka makao makuu ya wilaya ya Mbinga.Kata ya Mbuji ina jumla ya wakazi 11296 ambapo wanaume ni 4817 na wanawake ni 6452, ina vijiji 5 (Mbuji, Litembo, Kitura,Nyoni na Mpapa.).Kata ya Mbuji ina shule za msingi 5(MBUJI, KILANGA JUU,MYAU, KIBANGA na MAWONO) na sekondari moja. Mbuji sekondari inayo milikiwa na serikali. Pia kuna zahanati moja iliyofunguliwa na mwenge mwaka 2014,kata ya Mbuji ina mradi wa maji ambao umefadhiriwa na serikali jumla.... wanategemea kunufaika na mradi huo.
Sehemu kubwa ya wakazi ya kata hii ni wakulima wa mazao ya chakula,wakilima zaidi mihogo,ngano,mahindi na maharage na Kahawa kama zao la biashara
Pia sehemu kubwa ya kata ya Mbuji inamawsiliano ya simu za mikonononi kutoka kwa makampuni ya vodacom,tigo na airtel.Kata hii pia ipo katika mpango wa umeme vijijini ambapo apaka December 2014 inatarajiwa kutakuwa na Umeme. Tembelea ukurasa wa utalii(tourism) ili uone utalii ndani ya mbuji
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit