Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura amewapongeza wananchi wa Kata ya Mkako kwa kuunga mkono jitahada zinazofanywa na Serikali za kuwaondolea adha wanafunzi kutembelea umbali mrefu kufuata elimu.
Wananchi wa Kata ya Mkako wametoa eneo la ekari 7 liliopo katika Kitongoji cha Muungano Kijiji cha Lihale kwa ajili ya kujenga shule shikizi,wananchi hao wanatekeleza ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na ofisi 1 utekelezaji ambao upo katika hatua ya renta.
Mkurugenzi Kashushura ametoa pongezi hizo katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata hiyo tarehe 09 Septemba 2024.
Amesema “Huu ni utekelezaji wa kimkakati madarasa haya yakikamilika yatawaondolea adha hawa wanafunzi ambao wanatembea umbali mrefu ni ahidi kuongeza nguvu hasa katika upande wa simenti na nondo ili mradi huu ukamilike”
Pamoja na ahadi hiyo Mkurugenzi Kashushura ameahidi kutoa Shilingi Ml. 5 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Lihale.
Kwa upande wake Afisa Elimu Kata Kata ya Mkako France Komba amebainisha kuwa ujenzi huo wa shule shikizi unatarajia kukamilika mapema ili ifikapo Januari 2025 shule hiyo ianze kutoa huduma kwa wanafunzi ambao wanatembea zaidi ya kilometa 5 kwenda katika shule mama.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit