Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbinga Ndg. Joseph Mdaka amewapongeza madiwani wa Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika maeneo yao.
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 4 Februari 2024 katika maadhimisho ya miaka 47 ya chama cha mapinduzi yaliyofanyika Kiwilaya katika Kata ya Maguu Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
" Niwapongeze sana madiwani wote wa Wilaya ya Mbinga mnafanya kazi kubwa na inaonekana, endeleni kushirikiana na wataalam katika kuwaletea wananchi maendeleo" Amebainisha Mdaka
Aidha Mdaka amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule ili waweze kupata elimu, amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ya elimu ili boresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amewataka wananchi wa Wilaya ya Mbinga kuhakikisha wanaimarisha amani katika maeneo yao hasa katika kipindi tarajiwa cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
" Amani ni msingi wa kuleta maendeleo katika nchi yetu sehemu yoyote isiyo na amani haina maendeleo, tuilinde amani yetu" Amesisitiza Mangosongo
Imeandikwa na Silvia Ernest
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
5 Februari 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit