• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima

MBINGA DC KUWA MFANO UTEKELEZAJI WA MRADI MKUBWA WA UMILIKISHAJI ARDHI NCHINI

Tarehe ya kuwekwa: January 11th, 2023

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa Kuboresha Miliki za Ardhi kwenye vijiji 50 kati ya 117 vya Halmashauri hiyo kuanzia mwaka huu wa fedha 2022/2023.

Katika Kikao cha kutambulisha mradi kilichoongozwa na Maafisa wa Wizara ya Ardhi leo Jumatano Januari 11, 2023 katika Ofisi za Halmashauri Kiamili na kukutanisha pia Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma, Maafisa Ardhi, Wakuu wa Idara na Vitengo na Timu ya Utekelezaji wa mradi ngazi ya Halmashauri, Meneja wa Mradi Taifa Bw. Joseph John Osena amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni miongoni mwa Halmashauri 41 za mfano zitakazoanza utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitano kati ya Halmashauri zote 184 nchini.

Bw. Osena amefafanua kuwa pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambayo ni Halmashauri pekee ya mfano kwa Mkoa wa Ruvuma katika awamu hii ya kwanza ya utekelezaji wa mradi kuna Halmashauri nyingine 40 kutoka Mikoa ya Arusha, Pwani, Simiyu, Tanga, Tabora, Geita, Kigoma, Mara, Shinyanga, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Songwe na Katavi na kwamba katika utekelezaji wake katika Halmashauri hizo Serikali inakusudia kuandaa, kumilikisha na kugawa jumla ya Hatimiliki za Ardhi (CROs) na Leseni za Makazi Milioni 2 kwenye maeneo ya mijini na Hatimiliki za Kimila (CCROs) 500,000 kwa maeneo ya vijijini.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi ngazi ya Halmashauri Bw. Maurus Hyera amesema kupitia mradi huo shughuli mbalimbali zinatarajiwa kuanza utekelezaji wake hivi karibuni ambazo zitahusisha uboreshaji wa Ofisi za Baraza la Ardhi la Wilaya, uboreshaji wa masijala za ardhi za vijiji, pamoja na uandaaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi (Land Use Plans) ngazi ya Wilaya lakini pia kwenye vijiji vyote 50 vya mradi.

Vilevile mradi utahusisha zoezi la upimaji wa mipaka ya vijiji utaoambatana na uandaaji na ugawaji wa Vyeti vya Ardhi kwa kila kijiji cha mradi lakini pia kushughulikia suala la usalama katika umiliki wa ardhi ambapo zaidi ya Hatimiliki za Kimila 40,000 zitaandaliwa na kugawiwa kwa wananchi.

Imeandikwa na

Salum Said 

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 

Tarehe 11 Januari, 2023

Matangazo

  • MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 18, 2022
  • MAELEKEZO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA SHULE ZA BWENI 2023 December 18, 2022
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI ENEO LA KIAMILI October 13, 2021
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MBINGA DC KUWA MFANO UTEKELEZAJI WA MRADI MKUBWA WA UMILIKISHAJI ARDHI NCHINI

    January 11, 2023
  • MBINGA DC YAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA MAPYA 10

    January 06, 2023
  • BENKI YA NMB YAWEZESHA PIKIPIKI KWA MAAFISA USHIRIKA MBINGA NA NYASA

    December 30, 2022
  • KAMATI YA SIASA YATEMBELEA KITUO CHA AFYA MKUMBI

    December 29, 2022
  • Tazama zote/kote

Video

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Christine Mndeme aagiza Halmashauri ya Wilaya kuhamiamia Kiamili kabla ya tarehe 30/10/2019
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya Mkoa wa Iringa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri Wilaya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Songea

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit