Katika mwaka wa fedha 2023/2024 ulioshia mwezi Juni 2024, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imevuka lengo katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya jumla ya Tshs. 7,757,338,926 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani.
Hayo yamebainishwa tarehe 27 Agosti 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu CPA. Samwel Marwa katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kujadili taarifa za hesabu za Halmashauri.
Amesema, kwa mwaka huo wa fedha Halmashauri iliidhinishiwa kukusanya Tshs. 6,300,000,000 ambapo hadi kufikia mwezi februari kiasi cha Tshs. 5,050,776,560.11 kilikusanywa sawa na 80% ya makusanyo.
“Jumla ya shilingi Tshs. 6,885,663,457 ni makusanyo ya kodi na tozo,faini, Tshs.16,342,373 ni faini,leseni na ada, Tshs. 855,333,096 haya ni mapato mengineyo” Amebainisha CPA. Marwa
Aidha Marwa amebainisha kuwa Halmashauri ilipokea fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu pamoja na wahisani Tshs. 38,138,622,344 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri zikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ameeleza kuwa kwa mwaka huo wa fedha , Halmashauri imetumia jumla ya Tshs. 43,822,590,229 fedha kutoka Serikali Kuu, Wahisani pamoja na mapato ya ndani katika kulipa stahiki za watumishi , matumizi ya ofisi, matengenezo, gharama za uchakavu wa mali pamoja na matumizi mengineyo.
Amesema “Stahiki za watumishi Tshs. 29,501,438,527, matumisi ya ofisi Tshs. 8,020,537,233, matengenezo Tshs. 695,547,891, matumizi mengineyo Tshs.99,711,000, fedha zilizohamishwa ngazi ya jamii Tshs. 937,568,916 pamoja na gharama za uchakavu wa mali Tshs. 1,102,793,977”
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit