• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

RC RUVUMA ATOA WITO WANUFAIKA TASAF KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Tarehe ya kuwekwa: January 18th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jen Wilbert Ibuge ametoa wito kwa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF Wilayani Mbinga kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa kupitia mpango huo kwa kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

RC Ibuge ametoa wito huo leo Januari 18, 2022 wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Amanimakolo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambapo amepokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango kwenye Kata ya Amanimakolo na kutembelea kaya za walengwa na wanufaika wa Mpango huo kijijini hapo.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema wanufaika wanapaswa kutambua na kuthamini uzito wa kile wanachokipokea kupitia TASAF na kwamba fedha hizo zitekeleze na kutumika kama zilivyokusudiwa ikiwemo kugharamia mahitaji ya watoto shuleni na bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) huku  akipongeza jitihada zilizofanyika kuwezesha asilimia 77 ya kaya zote za wanufaika wa TASAF wilayani Mbinga kujiunga na mfuko huo.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini Wilayani Mbinga, Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Aziza Mangosongo amesema kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Oktoba 2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilipokea jumla ya shilingi 908,398,800 kwa ajili ya malipo kwa kaya 8,669 zinazonufaika na Awamu ya Tatu, Kipindi cha Pili cha utekelezaji wa Mpango huo kutoka kwenye vijiji vyote 117 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

Aidha, Mhe. Mangosongo amefafanua malengo ya mpango huo wa TASAF kuwa ni kuziwezesha kaya masikini kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji ya msingi kama chakula, afya, malazi, elimu na makazi, sambamba na kupokea ruzuku ya masharti kwa watoto kuhudhuria shule na kliniki.

Akielezea namna wananchi wanavyonufaika na mpango wa TASAF na mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wake kwenye vijiji vya Amanimakolo, Kiwombi na Mkeke vilivyopo Kata ya Amanimakolo Bw. Joachim Ngaponda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata hiyo amesema mpango huo umechangia kuongezeka kwa mzunguko wa fedha na msukumo wa shughuli mbalimbali za kiuchumi vijijini, ongezeko na hamasa ya jamii kujiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa

Bw. Ngaponda ameongeza kuwa mpango huo wa kusuru kaya masikini umechochea kuimarika kwa mahudhurio na kupungua kwa utoro wa vipindi kwa wanafunzi wa  shule za msingi na sekondari, huku mmoja wa wanufaika wa mpango huo Bi Orenata Markus Haule akieleza kuwa kupitia ruzuku anayopokea kupitia TASAF amefanikiwa kugharamia mahitaji ya shule kama vile sare za shule, viatu na mahitaji mengine jambo ambalo kabla ya mpango lilikua gumu kwa upande wake kutokana na hali duni ya maisha aliyokua nayo.

Imeandikwa na Salum Said

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga 

Tarehe 18 Januari, 2022



Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit