Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jen. Wilbert Ibuge ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono utelelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kujitolea nguvukazi zao ili kuunga mkono jitihada za serikali na kuharakisha ukamilishaji wa miradi hiyo.
Akizungumza na wananchi leo Novemba 25 wakati wa hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ruanda ambapo alialikwa kama Mgeni Rasmi RC Ibuge amesema anatambua na kupongeza jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na wananchi katika kuchangia na kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo na kwamba wao kama wananchi ni lazima wawe chachu na sehemu ya maendeleo yao wenyewe kwani serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu
Ameongeza kuwa pamoja na serikali kuwa na mipango endelevu ya kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezwa kwa kasi na ubora uliokusudiwa lakini ni ukweli usiopingika kuwa nguvu za wananchi zinapoingia na kujumuishwa husukuma na kuongeza kasi ya utekelezaji na ukamilishaji wa miradi hiyo.
Naye Bi. Fransis kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Ruanda ameshukuru serikali na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kufanikisha ukamilishaji wa Zanahati hiyo ambayo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2013.
Amesema pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo lakini wao kama wananchi wanatambua kuwa bado kuna changamoto ya ukosefu wa nyumba za watumishi na kwamba tayari wameandaa benki tofali za kutosha na kuahidi kuwa kujitolea nguvukazi zao kuanza kutekelezaji ujenzi wa nyumba hizo za watumishi huku wakiomba serikali kuwaunga mkono wa kuwapatia vifaa vya viwandani kama bati, saruji, misumari na rangi.
Pamoja na kufungua Zahanati ya Ruanda, Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari za Ruanda, Mkako, Kiamili na Shule ya Sekondari ya Wasichana Mbinga ambapo mara baada ya kujionea hatua iliyofikiwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia vema miradi hiyo katika kusimamia miradi hiyo na kwamba ni matarajio yake miradi yote inayotekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo itakamilika kwa ubora na haraka ndani ya muda uliokusudiwa.
Imeandikwa na
Salum Said,
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
25 Novemba 2021
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit