• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

NBC KUANZA KUHUDUMIA WATUMISHI MBINGA DC

Tarehe ya kuwekwa: April 23rd, 2021

Benki na Taifa ya Biashara, NBC imeingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wa makubaliano ya kutoa huduma za kifedha kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.

Akizungumza kwenye kikao cha wawakilishi wa NBC na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kilichofanyika leo Aprili 23 Ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji Kiamili, Meneja Maendeleo ya Biashara wa benki ya NBC, Kelvin Kisyima amezungumzia juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na huduma za mikopo kwa watumishi, bima za aina zote, na akaunti mahsusi kwa wajasiriamali, wakulima na watumishi.

Jennifer Peter na Leonia Haule ambao ni maafisa Mikopo wa NBC wameongeza kuwa benki hiyo imetoa ofa na punguzo maalumu la riba kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga watakaochukua mikopo kupitia benki ya NBC na kwamba mikopo yote itatozwa riba ya 16% tu kwa mwaka, kiwango cha mkopo kikianzia Milioni 1 hadi Milioni 125 huku muda wa kurejesha ukiwa ni hadi miaka 6.

Benki ya NBC imewahakikishia watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kutoa huduma za kipekee, uwazi na utoaji wa huduma za akaunti zenye gharama nafuu za uendeshaji kwa kulinganisha na gharama zinazotolewa na taasisi nyingine za kifedha na kwamba huduma ya mkopo ni kwa watumishi wote hata wale ambao mishahara yao haipitii benki ya NBC.

Kwa upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo waliopata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao waliomba benki hiyo kupanua huduma zake kwa kufungua tawi na kuongeza vituo vya kutolea huduma wilayani Mbinga huku Mkuu wa Idara ya Utumishi, Bw. Mfaume Cassim akitoa rai kwa benki hiyo kuzingatia utoaji wa huduma zake hasa za mikopo kwa watumishi wenye sifa na wanaostahili kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

Bw. Kelvin Ksyima amefafanua kuwa kwa sasa benki ya NBC imeweka mkakati wa kuwafikia wateja kwa urahisi na kwamba kwa sasa huduma zote wilayani Mbinga zinapatikana kupitia Wakala Mkuu (Super Agent) lakini pia kupitia mawakala wadogo 7 waliopo Mbinga mjini na kueleza kuwa beniki hiyo ina mpango wa kuongeza wakala mwingine eneo la Kigonsera.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Juma Mnwele, ameihakikishia benki ya NBC kuwa milango ipo wazi na kwamba Ofisi yake kupitia Wakuu wa Idara, Vitengo na Wakuu wa Vituo vya kazi inaahidi kutoa ushirikiano muda wowote ikiwemo kuthibitisha usahihi wa taarifa za watumishi wakati benki hiyo itakapohitaji kufanya uhakiki wa taarifa za watumishi watakaohitaji mikopo.


Imeandikwa na:

Salum Said

Afisa Habari

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA.  Aprili 23, 2021

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit