KATA YA MPAPA .
Kata ya Mpapa ipo umbali wa km ....... toka makao makuu ya wilaya ya Mbinga.Kata ya Mpapa ina jumla ya wakazi 10425 ambapo wanaume ni 5006 na wanawake ni 5419, ina vijiji 5 (Buruma, Mitawa, Mpapa, Chunya na Mitanga).Kata ya Mpapa ina shule za msingi 8(Burma,Mitanga,Mpapa,Safina,Kiwalangi,Arusha na Chunya) na sekondari moja. Miparu sekondari inayo milikiwa na serikali. Pia kuna zahanati moja iliyofunguliwa na mwenge mwaka 2014,kata ya Mpapa ina mradi wa maji ambao umefadhiriwa na serikali jumla.... wanategemea kunufaika na mradi huo.
Sehemu kubwa ya wakazi ya kata hii ni wakulima wa mazao ya chakula,wakilima zaidi mihogo,ngano,mahindi na maharage na Kahawa kama zao la biashara
Pia sehemu kubwa ya kata ya Mpapa inamawsiliano ya simu za mikonononi kutoka kwa makampuni ya vodacom,tigo na airtel.Kata hii pia ipo katika mpango wa umeme vijijini ambapo apaka December 2014 inatarajiwa kutakuwa na Umeme. Tembelea ukurasa wa utalii(tourism) ili uone utalii ndani ya mbuji.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit