Katika Mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilitenga na kutumia fedha kiasi cha shilingi 1,544,770,750.00 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za afya.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe George Mhina tarehe 15 Julai 2025 katika kikao cha tathmini ya utoaji wa huduma za afya Hamashauri ya Wilaya ya Mbinga katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Ameeleza kuwa pamoja na mapato ya ndani Halmashauri ilipokea fedha kutoka Serikali Kuu shilingi 1,516,725,927.17 kwa ajili ya utekelezaji huo.
Fedha hizo zimetumika kuboresha miundombinu ya Zahanati 18, Vituo vya Afya 4 pamoja na miundombinu ya Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit