Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura ametoa rai kwa Watendaji wa Kata,Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji wa Kata zilizopokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kushirikiana kwa pamoja wakati wa utekelezaji wa miradi ili kuleta umiliki na ubora wa miradi inayotekelezwa.
Rai hiyo imetolewa tarehe 29 Julai 2025 katika kikao kazi kilichohusisha Timu ya Menejimenti ya Halmashauri, Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga juu ya mapokezi ya fedha na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
“Hii miradi yetu sisi Serikali imeleta fedha kwa ajili ya utekelezaji naomba sana mkahamasishe wananchi kwenye maeneo yenu ili tushirikiane kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi” Amesisitiza
Amefafanua kuwa ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa miradi unaleta umiliki wa miradi kwa wananchi wa eneo husika pamoja na kupunguza baadhi ya gharama za utekelezaji wa miradi.
Akichangia mada Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahilo Asili Kata ya Mbuji Claudius Miringa amemshukuru Mkurugenzi kwa kuandaa na kuitisha kikao cha utekelezaji akisisitiza kuwa haijawahi kutokea tangu aingie madarakani,ameahidi kutoa ushirikiano na kuhamasisha wananchi kushiriki utekelezaji huo.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Lukarasi Joseph Ndunguru amethibitisha kuwa kikao hicho ni chachu katika kuleta uelewa wa pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit