ELIMU YA MSINGI.
Afisa Elimu Msingi: Mr. Samwel Komba |
Wilaya ya Mbinga ina jumla ya Shule za Msingi 227 zenye jumla ya wanafunzi 79,473 kati yao wavulana ni 39,033 na wasichana 40,440. Aidha kati ya Shule 227, Shule 5 ni za binafsi zinazomilikiwa na Madhehebu mbalimbali ya dini zenye jumla ya wanafunzi 1,106 wakiwemo wavulana 549 na wasichana 557 .Wilaya ina Shule mbili zinaozojumuisha kundi maalum la wanafunzi wenye ulemavu wa Viungo, Akili na Ngozi (Albino). Shule hizo ni St. Wilhelm na Huruma.Wilaya ina jumla ya Walimu ........ ambapo wanawake .....na wanaume........
MAFANIKIO
Halmashauri iliyoongoza kufanya vizuri kitaifa katika mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 na hivyo kuzawadiwa Ngao ya Halmashauri bora kitaaluma mwaka 2013
Halmashauri ambayo ilitoa shule nyingi zipatazo 109 zilizofanya vizuri na kuzawadiwa vyeti vya shule zilizoongoza ufaulu kitaifa.
Wanafunzi wote wanakula shuleni chakula cha mchana,hii imesaidia sana kwa sasa kwani utoro umepungua kwa asilimia 90. Hivyo kuongeza ufaulu kwa darasa la nne nadarasa la saba
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit