Wataalam kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) wameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga hususan ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya Elimu.
Hayo yamebanishwa Juni 17, 2025 na Bw. Robert Sabwoya Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambae pia ni kiongozi wa ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
“Niwapongeze sana tumeridhishwa na utekelezaji wa miradi hii mfano hii shule ya Sekondari Mashujaa mmetekeleza kwa kutumia force account lakini ni kama mmetumia kandarasi, niwapongeze sana” Amebainisha
Naye Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu na Maendeleo ya Miji na Vijiji Mhandisi Neema Mbilinyi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ameeleza kuwa moja ya changamoto kubwa wakati wa utekelezaji wa miradi ni jeographia ya Wilaya ya Mbinga yenye miinuko na mabonde inayopelekea kuongezeka kwa gharama za utekelezaji.
“Tunashukuru sana Serikali kwa kutuletea fedha lakini changamoto tunayokumbana nayo sana ni kuongezeka kwa gharama za miradi kama mlivyoona wenyewe tunaomba mtufikirie wakati wa kuleta fedha kwa ajili ya utekelezaji” Amebainisha
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari MMwalimu Felix Danda amesema moja ya mafanikio ya utekelezaji wa miradi sekta ya Elimu ni kuwaondolea adha wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule maeneo jirani.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 5 na matundu ya vyoo Shule ya Msingi Lunoro, Jengo la uwekezaji (Mbinga DC Mall), Shule mpya Sekondari Mashujaa, Ujenzi wa mabweni 2 Shule ya Sekondari Hagati pamoja na ujenzi wa vymba 7 vya madarasa Shule ya Msingi Ukata.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit