Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ni miongoni mwa Halmashauri 8 za Mkoa wa Ruvuma.Halmashauri hii inapatikana katika Wilaya ya Mbinga, Makao yake Makuu yakipatikana eneo la Kiamili Kata ya Kigonsera takribani umbali wa kilometa 32 kutoka Mbinga Mjini na Kilometa 67 kutoka Songea Mjini na Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina eneo la ukubwa wa kilometa za mraba 6,319.31, Tarafa 5, Kata 29, Vijiji 117.Kwa upande Kusini na Magharibi halmashauri imepakana na Wilaya ya Nyasa, Halmashauri ya Wilaya Mbinga Mjini na Wilaya ya Songea kwa upande wa Mashariki na Wilaya ya Ludewa (Mkoa wa Njombe) kwa upande wa Kaskazini.
Hali ya hewa ya Mbinga ni joto la wastani wa 25°C. Wakati wa kiangazi hali ya joto inakuwa nyuzi 23oC hadi 27oC na wakati wa baridi kiasi cha joto huwa kuanzia 160C hadi 200C. Mvua hunyesha kwa muda wa miezi sita kuanzia Novemba hadi April. Wastani wa mvua ni mm. 1,200 – mm 1,800 kwa mwaka, hata hivyo katika Milima ya Umatengo wastani wa mvua hufikia mm 2,000 kwa mwaka. Aidha, kipindi cha kiangazi ni kuanzia Mei hadi Oktoba..
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022 ,Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina wakazi 285,582 kati yao wanaume ni 141,271 sawa na 49.5% na wanawake ni 144,311 sawa na 50.5%.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit