Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Jumanne Aprili 20 imeanza ziara ya siku mbili ya kutembelea na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Desderius Haule imeanza ziara hiyo Jumanne Aprili 20 kwa kutembelea miradi iliyopo Kata za Ruanda, Namswea, Litumbandyosi na Amani Makolo.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo kwa siku hii ya kwanza ni Shule mpya ya Sekondari ya Wavulana Mbinga (Mbinga Boys), ambayo imefunguliwa mwaka huu 2021, mradi wa Bweni Shule ya Sekondari Ruanda, Zahanati ya Ruanda, ujenzi wa madarasa Shule ya Msingi Mabuni na Shule ya Msingi Ntunduwaro pamoja na Madarasa mawili ya Shule ya Msingi Mtazamagama, Amani Makolo.
Kamati hiyo ya Fedha itaendelea na ziara yake Jumatano hii Aprili 21 kwa kutembelea Shule mpya ya Sekondari Kipapa ambayo pia imefunguliwa mwaka huu 2021, Kituo cha Kilimo Maguu, eneo la ujenzi wa shule maalumu Maguu, mradi wa vijana wa kiwanda cha sabuni Kata ya Mapera, na mradi wa ujenzi wa bweni na madarasa Shule ya Sekondari Litembo.
Imeandikwa na;
Salum Said,
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit