Halmashauri ya Wilaya Mbinga imefanya mnada wa kahawa kwa mara yakwanza ndani ya Halmashauri, mnada huu ni matokea ya agizo la Waziri mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mh: Kassim Majaliwa alipofanya ziara Wilaya ya Mbinga, januari 2019. Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza mnada wa kahawa ufanyike kwenye kanda ambazo kahawa huzalishwa.
Wilaya ya Mbinga imeweza kutimiza agizo hilo ambapo Mbinga inakuwa makao makuu ya kanda ya Ruvuma huku kahawa kutoka Nyasa, Madaba na Songea ikiletwa hapa kwaajili ya Mnada
Katika ufunguzi wa mnada kwa mara ya kwanza Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ametaka wafanyabiashara na makampuni mbali mbali kujitokeza nakushiri katika mnada huo, mnada kwa Mbinga utafanyika kila alhamis.
Katika mnada wa leo jumla ya magunia 15287 yenye kilo 60 kila moja yameuzwa kwa mnada sawa na kilo 917,220. Jumla ya fedha inaandaliwa kwakuwa makampuni bado yanafanya majumuisho ya ununuzi wa kahawa hiyo.
Pichani: Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bwana Juma Mnwele akifuatilia mnada wa kahawa
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit