Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuri akiwa ziarani Mkoani Sumbawanga aliagiza kila Halmashauri ambayo inafanya kazi nje ya eneo lake la utawala ihamie kwenye eneo lake la utawala kabla ya tarehe 07/11/2019.
Mheshimiwa Mkuuu wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme aliitisha baraza la dharula lililofanyika tarehe 22/10/2019 nakuagiza Halmashauri ihamie kwa muda katika eneo la Kigonsera kabla ya tarehe 30/10/2019
Aidha maamuzi haya yalikuja baada ya mapendekezo ya baraza la madiwani kutaka Halmashauri kuhamia moja kwa moja katika kata ya Mkumbi, Mkuu wa mkoa alipofanya ziara na kutembelea miji ya Mkako ambapo kijiji kilitoa ekari 69, kata ya Kigonsera katika eneo la Kiamili kuna ofisi ya Serikali na eneo lililotolewa na Kijiji la ekari 100. Eneo la mwisho kutembelea lilikuwa ni kata ya Mkumbi ambapo kijiji cha Mkumbi kilitoa ekari 15 na kijiji cha Longa kilitoa ekari 30. Baada ya kupitia maeneo hayo na kuangalia muda wa kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais, aliamuru ofisi za muda zihamie Kigonsera wakati wataalam na Madiwani wakitafuta eneo la kujenga ofisi za kudumu.
“Kwa sasa ofisi za muda za Halmashauri zihamie Kigonsera kwa kuwa kuna Ofisi za serikali na nyumba ya Mkurugenzi” alisema, Pia akatoa rai kuwa baraza la madiwani linajukumu la kutafuta eneo la kujenga ofisi ya kudumu, eneo la kujenga ofisi za kudumu litatakiwa lisiwe chanzo cha maji, liangalie miundombinu kama umeme, mkongo na eneo huru ambalo sio la fidia, alisisitiza mkuu wa mkoa.
Pia Mheshimiwa mkuu wa Mkoa ameahidi kutoa magari ili kuhakikisha kabla ya tarehe 30/10/2019 tayari ofisi zianze kutoa huduma katika eneo la utawala ambalo ni Kigonsera katika majengo ya shule ya wasichana ya Mbinga
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit