Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekua Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Cosmas Nshenye katika hafla iliyofanyika leo Juni 29, 2021
Hafla hiyo ya makabidhiano ya ofisi imefanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote mbili za Mji na Wilaya ya Mbinga, Wakuu wa Taasisi, Idara na Vitengo, viongozi wa dini, wawakilishi kutoka sekta binafsi na watumishi wengine.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo amesema ni furaha kubwa kwake kujumuika na wanambinga na anategemea kupata ushirikiano na mshikamano kutoka kwa viongozi na wananchi ili kusongesha mbele gurudumu la maendeleo ya Wilaya ya Mbinga na Taifa kwa ujumla.
Naye Mhe. Nshenye ametoa shukrani zake kwa viongozi na wananchi wa wilaya ya Mbinga kwa ushirikiano mkubwa alioupata kwa kipindi chote alichofanya kazi na kuwahudumia wananchi wa Mbinga
Makabidhiano haya ni kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyofanywa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanya teuzi za Wakuu wa Wilaya ambapo Mhe. Nshenye ambaye hapo kabla alikua Mkuu wa Wilaya ya Mbinga alihamishiwa Mkoani Songwe na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi.
Pia Mhe. Suluhu alimteua Mhe. Aziza ambaye hapo awali alikua Mkuu wa Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara na kumhamishia Wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma kuchukua nafasi ya Cosmas Nshenye.
Imeandikwa na
Salum Said,
Afisa Habari, Mbinga D.C
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit