Mapema leo tarehe 18 Aprili 2024, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Rwiza ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya unaotekelezwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Baadhi ya majengo aliyotembelea katika hospitali hiyo ni pamoja na jengo la utawala, maabara, jengo la kufulia pamoja na jengo la mama na mtoto.
Aidha Mkurugenzi Rwiza ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambao upo katika hatua za ukamilishaji.
Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha usimamizi katika utekelezaji huo ambao utakwenda kuleta tija kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kama ilivyo azma ya Serikali.
Imeandikwa na Silvia Ernest,
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Tarehe 18 Aprili 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit