Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Rwiza amewataka Walimu Wakuu wa shule za Msingi na Wakuu wa shule za Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuhakikisha wanaweka kisanduku cha huduma ya kwanza( First Aid Kit) shuleni ili kuwezesha utoaji wa huduma ya kwanza kwa wanafunzi.
Agizo hilo limetolewa tarehe 19 Aprili 2024 katika kikao kazi cha Mkurugenzi Mtendaji na walimu Wakuu na Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Tarafa pamoja na Watendaji wa Kata.
" Uwepo wa first aid kit katika shule zetu ni muhimu sana katika kutoa huduma ya kwanza kwa wanafunzi wetu pindi dharula inapotokea ,kwahiyo kila Mkuu wa shule ahakikishe anatekeleza hili" Amebainisha Mkurugenzi Rwiza
Ili kuhakikisha wanafunzi wanaongeza maarifa na ustadi amewataka walimu hao kuanzisha na kuendeleza klabu mbalimbali katika shule zao akisisitiza kuwa ni mfumo mzuri wa kuwajengea uwezo pamoja na kuwaongezea maarifa wanafunzi.
" Kuna Klabu kama za mazingira, Rushwa na nyingine nyingi anzisheni hizi Klabu na kama zipo basi ziendelezeni zina faida kubwa kwa wanafunzi"Amesisitiza
Aidha katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na katika ubora tarajiwa amewataka washiriki wa kikao hiko kushirikiana kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi pamoja na kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi.
Kwa upande wa Maafisa Elimu Kata, Mkurugenzi Rwiza amewataka maafisa hao kutimiza wajibu wao wa kusimamia na kufuatilia masuala ya taaluma katika maeneo yao lengo likiwa ni kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Imeandikwa na Silvia Ernest
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Tarehe 19 Aprili, 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit