Uanzishaji wa Viwanda: Wilaya ya Mbinga inazalisha mazao mbalimbali kwa kiasi kikubwa ambapo wawekezaji wanaweza kuwekeza kwa kujenga maghala na Viwanda.
Kiwanda cha kusindika kahawa na Ghala la kuhifadhi kahawa. Wilaya ya Mbinga inazalisha Kahawa kwa kiasi kikubwa sana, na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inazalisha Kahawa takribani Tani 17,312 kwa Mwaka na Viwanda na maghala vinavyotegemewa ni vile vilivyopo katika Halmashauri ya Mji tu, hivyo basi tunawaalika wawekezaji mbalimbali waweze kuja kuwekeza katika Wilaya yetu kwa kujenga viwanda na Maghala kwa zao la Kahawa. Aidha maeneo ya kujenga viwanda na maghala yanapatikana katika Kata za Nyoni,Mbuji,Miyau na Mkumbi.
Kiwanda cha kusindika Sembe: Wilaya ya Mbinga inazalisha Mahindi kwa kiasi kikubwa sana, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inazalisha Mahindi Takribani Tani 124,080 kwa mwaka. Hivyo basi wawekezaji mbalimbali wanaalikwa kwa ajili ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kusindika Sembe katika Wilaya ya Mbinga. Maeneo rafiki na yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda hivi ni Kigonsera, Mkako, Ruanda na Matiri.
Kiwanda cha kusindika bidhaa za zao la Soya. Wakulima wa Wilaya ya Mbinga wamehamasika na kulima zao la Soya kwa wingi sana,kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga takribani Tani 2,363.5 zinazalishwa. Hivyo basi tunawahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika zao la Soya na mazao yake yote kama Chakula cha Kuku,Maziwa ya Soya na Unga wa Lishe. Maeneo rafiki na yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda hivi ni Kigonsera,Amani Makolo Mkako, Ruanda na Matiri.
NB: Jumla ya Ekari 351.6 za uwekezaji wa viwanda zimeainishwa.
Ujenzi wa Hoteli na Nyumba za kulala wageni: Wilaya ya Mbinga ina maeneo mengi kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli na Nyumba za kulala wageni. Kwasasa ujenzi wa majengo haya umekuwa ni fursa kubwa kwa miji yetu inaendelea kukua na uhitaji umekuwa ni mkubwa kutokana na ongezeko la watu. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Kijiji cha Kigonsera kuna Ekari …. Kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo hiyo basi wawekezaji wanakaribishwa ili waweze kuwekeza.
Uendelezaji wa zao la Korosho: Wilaya ya Mbinga imejikita katika ulimaji wa zao la Korosho. Idadi ya wakulima wanaolima mpaka sasa ni 1576, idadi ya miti iliyopandwa mpaka sasa ni 300,052, hekta zilizolimwa ni 4,500 kati ya hekta 14,500 zinazofaa kwa kilimo cha Korosho. Uzalishaji unakadiriwa kuwa wa wastani wa Tani 47.52 kwa mwaka.
Maeneo mengi ni ya watu binafsi na baadhi ya maeneo ni ya Serikali za vijiji ambapo Zaidi ya Ekari 2000 zinapatikana katika Serikali ya Vijiji ndani ya Kata za Ruanda na Litumbandyosi.
Upatikanaji wa mbegu na miche ya Korosho. Miche inapatikana kutoka katika kituo cha utafiti wa Kilimo “TARI NALIENDELE MTWARA” katika mashamba yake yaliyoko maeneo mbalimbali katika kanda ya kusini ikiwepo na shamba la Paradiso lililopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Kwa maelezo haya mafupi Wilaya ya Mbinga inawakaribishara wawekezaji mbalimbali ili muweze kuwekeza katika zao hili la Korosho ambapo kata za Ruanda, Litumbandyosi na Kihungu ndizo zinazolima zao hili kwa Wilaya ya Mbinga.
Uwekezaji katika Makaa ya Mawe:
Wilaya ya Mbinga imebarikiwa kuwa na mashapo ya makaa ya mawe ambapo inakadiliwa kuwa kuna jumla Tani 367 kwa eneo la Mbuyula - Mkapa na Mbalawala. Hata hivyo kiasi cha mashapo ya makaa ya mawe yanatarajiwa kuongezeka kutokana na tafiti mpya kuonyesha uwepo wa makaa ya mawe kwa eneo la kijiji cha Paradiso. Kwa sasa upatikanaji wa vitalu kwenye eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inategemea na hatua za utafiti (Geological survey). Upatikanaji wa Leseni za vitalu vya madini usimamiwa na Tume ya Madini.
Zipo fursa mbalimbali katika sekta ya uchimbaji wa makaa ya mawe ambazo zinajumuisha maeneo yafuatayo:-
Kumiliki Vitalu vya Makaa ya Mawe.
Biashara ya uuzaji wa makaa ya mawe kwa masoko ya ndani na nje.
Biashara ya usafirishaji
Biashara ya bidhaa mbalimbali kama vipuli vya magari na mitambo
Biashara ya mafuta na vilainishi
Biashara ya vyakula
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit