Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga limeridhia na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wenye makadirio ya mapato na matumizi ya Tshs. 43,884,045,000.
Rasimu hiyo imewasilishwa katika Kikao maalum cha baraza kupitia randama ya bajeti ya matumizi ya kawaida na mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika tarehe 1 Februari 2024 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Kigonsera.
Mchanganuo wa makadirio hayo ni ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani Tshs. 8,400,000,000. ambapo mapato halisi ni Tshs. 6,800,000,000 na mapato fungwa ni Tshs. 1,600,000,000.
Mishahara ya watumishi Tshs. 23, 249,317,000, matumizi mengineyo Tshs. 1,163,116,000 pamoja na Tshs 11,071,612,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo fedha kutoka Serikali kuu.
Mikakati iliyokwekwa na Halmashauri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ni pamoja na kuongezwa kwa idadi ya POS za kukusanyia mapato, kukarabati Soko la Ruanda na Jengo la uwekezaji lililopo Mbinga Mjini ili kuchochea biashara zitakazopelekea kuongezeka kwa mapato.
Pia ukarabati wa stendi ya mabasi ya Ruanda na Maguu, ujenzi wa vibanda vya biashara, ukarabati wa kituo cha kukusanya mapato Kitai pamoja na ujenzi wa Shule ya msingi mchepuo wa kingereza( English Medium).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mhe. Deusderius Haule amewataka wataalamu na madaiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kushirikiana na kuimarisha usimamizi katika uukusanya mapato ili kuweza kufikia malengo ya Halmashauri.
imeandikwa na Silvia Ernest
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
1 Februari 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit