Kamati ya Siasa ya Wilaya, chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbinga Ndg. Joseph Mdaka imeendelea na ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Leo Jumanne Disemba 27 Kamati hiyo imetembelea Kata ya Kigonsera na kukagua maendeleo ya mradi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na Makao Makuu ya Halmashauri eneo la Kiamili, pamoja na mradi wa Madarasa Mawili yaliyojengwa na kukamilika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Mbinga.
Katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoanza Alhamisi Disemba 22 wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake imeoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi unaofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kupitia utekelezaji za miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wiki iliyopita Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbinga ilianza ziara yake kwa kutembelea mradi wa Shule Maalum ya Msingi ya Bweni kwa watoto wenye ulemavu inayojengwa Kata ya Maguu na leo imekagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mbinga na mradi wa Ofisi mpya za Mkurugenzi na Makao Makuu ya Halmashauri eneo la Kiamili, Kata ya Kigonsera.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit