Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma (alie simama pichani), akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya CHF iliyoboreshwa yaliyofanyika hivi karibuni ndani ya
Ukumbi wa Jimbo -Mbinga.
CHF iliyoboreshwa ni nini?
CHF iliyoboreshwa ni bima ya afya kwa ajili ya wananchi wa mikoa ya ya Tanzania bara ikiwepo mkoa wa Ruvuma ambao hawana uwezo au hawajatimiza vigezo vya kujiunga na bima ya afya ya taifa (NHIF).
Bima hii inaendeshwa na mfuko wa bima ya taifa (NHIF) kupitia ofisi za kwenye mikoa na Halmashauri zote ndani ya mkoa ndio wasimamizi wa CHF iliyoboreshwa.
CHF iliyoboreshwa imeanzishwa kuondoa changamoto zilizokuwepo kwenye mfuko wa afya ya jamii (CHF) ulioanzishwa mwaka 2001. Katika CHF iliyoboreshwa, huduma zinatolewa katika hospitali na zahanati za binafsi, mashirika ya dini na zile za serikali. Kupitia CHF ilyoboreshwa, mgonjwa atakuwa anauwezo wakutibiwa popote kwani mradi huu utafanya kazi kwa mifumo ya Kieletroniki na mgonjwa atatambulika popote alipo na hivyo kutatua kero ya mgonjwa kutibiwa ndani ya kituo kimoja alichojisajili.
Gharama ya kujiunga ni shilingi elfu thelasini (Tsh. 30,000) kwa kaya (mwanachama, mwenza wake na Watoto wanne) kwa ajili ya huduma kwa mwaka mmoja.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit