Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo leo Juni 6, 2023 ameongoza kikao cha maandalizi kuelekea kufanyika kwa maonesho ya Nane Nane mwaka huu 2023.
Kupitia kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mbinga (FDC) Mkuu wa Wilaya ameendelea kuhamasisha na kutoa wito kwa wadau kutoka sekta zote binafsi na za umma kuweza kushiriki katika maonesho ya Nane Nane ngazi ya Wilaya ambayo yatafanyika Kijiji cha Amanimakolo kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2023.
Pamoja na viongozi wa Wilaya na Halmashauri kikao hicho pia kimehudhuriwa pia na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wataalamu wa Halmashauri, viongozi wa idara, wakala na taasisi za umma, viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya tarafa, kata hadi kijiji, wadau kutoka sekta binafsi, vyama vya ushirika, makampuni na wadau wengineo.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Wilaya amewaongoza wajumbe wa kikao kupitia na kujadili taarifa za kamati mbalimbali za maandalizi ya maonesho hayo ambayo kwa mwaka huu 2023 ngazi ya Wilaya yanatarajiwa kufanyika Kata ya Amanimakolo kuanzia Agosti 1 hadi 8 2023.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit