Katika kuunga mkoni jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha lishe na kutokomeza udumavu nchini, Juni 04,2023 Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kupitia Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeendesha zoezi la kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kuwajengea wananchi tabia ya kunywa maziwa yenye viini lishe vya kutosha vya kuupa mwili mahitaji mhimu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Haruna Masige amebainisha kuwa maziwa yana viini lishe vya kutosha kama vile protini,vitamini, mafuta, wanga pamoja na madini ya calcium na phosphorus ambavyo ni mhimu sana katika ukuaji na kuboreshaji wa afya.
Zoezi hilo lilifanyika katika Shule za Msingi za Mahenge na Litembo zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit