Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga yaendelea na zoezi la usajili wa vitambulisho vya uraia (NIDA)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga inatekeleza zoezi la Taifa la usajili wa Vitambulisho vya Uraia. Zoezi hili limeanza rasmi tarehe 2/02/2018 baada ya uzinduzi kimkoa uliofanyika tarehe tarehe 5/Jna/2018 makao makuu ya mkoa huko Songea. Wilaya ya Mbinga ina jumla ya kata 38 ambazo kati ya hizo 19 zipo Halmashauri ya Mji na 29 zipo Halmashauri. Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Mbinga ina jumla ya wakazi 312591. Nida imeanza zoezi hili kwa kugawa katika tarafa zake, Hivyo imeanza katika tarafazifuatavyo 1.Tarafa ya Hagati yenye kata zifuatazo:Maguu,Langilo,Mapera,Mikalanga na Mkoha, tarafa ya Mbuji yenye kata za Litembo, Mbuji,Kitura na Mpapa, tarafa ya Kigonsera yenye kata za Mkako,Kigonsera,Amani Makoro,Matiri,Mhongozi,Kitumbalomo,Kihangi mahuka,Mhongozi.
Wananchi wanasisitizwa kuhakikisha kuwa wanashiriki zoezi hili muhimu kitaifa kwani vitambulisho hivyo vya Uraia vina faida kubwa ikiwa pamoja na kumtambulisha mwananchi kama raia halali wa Tanzania.Ofisi ya NIDA wilaya inachukua fursa hii kusisitiza kuwa bado inapita kata zilizo bakia na wanatarajia ifikapo May 15 watakuwa wamepita kata na vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit