Kampuni ya Halotel Tanzania imeushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kuichagua na kuifanya Kampuni hiyo inayotoa huduma ya mawasiliano nchini kuwa miongoni mwa Kampuni kuu zinazotoa huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo.
Hayo yamejiri leo Jumanne Disemba 27, 2022 wakati ujumbe kutoka Kampuni ya Halotel Mkoa wa Ruvuma ukiwakilishwa na Afisa Biashara wa Kampuni ya Halotel Keneth Wello na Bw. Saulo Essau Mponda ambaye ni Afisa Biashara Kitengo cha Halopesa Tawi la Ruvuma na kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halotel Mkoa wa Ruvuma ulipokabidhi zawadi na salamu za Kampuni kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika tukio lililofanyika kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji zilizopo Kiamili na kupokelewa na Mweka Hazina wa Halmashauri Bw. samwel Marwa, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Juma Haji Juma.
Akiwasilisha shukrani za Kampuni mara baada ya kukabidhi zawadi na salamu za Krismasi na Mwaka Mpya wa 2023 kwa Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Wello kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halotel Mkoa wa Ruvuma amesema wao kama Halotel, na moja ya Kampuni kubwa zinazotoa huduma za Mawasiliano Wilayani Mbinga wanatambua na kuthamini mchango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kama mdau wao muhimu katika kuchochea ukuaji wa Kampuni na sekta nzima ya Mawasiliano nchini kwa kipindi chote cha Mwaka 2022.
Naye Bw. Samwel Marwa, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ameishukuru Kampuni ya Halotel kwa hatua hiyo muhimu katika kuimarisha mahusiano na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Halmashauri na Kampuni hiyo ili kuhakikisha uendelevu katika upatikanaji wa huduma bora na za uhakika za mawasiliano hususani huduma ya internet kwenye eneo la Kiamili zilipo Ofisi na Makao Makuu ya Halmashauri, kwenye taasisi kama shule na vituo vya kutolea huduma za afya, vituo vya kukusanyia mapato na maeneo mengine ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Na Salum Said, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mbinga DC.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit