Wakuu wa Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuongoza Wilaya za Mkoa wa Ruvuma wameapishwa leo Juni, 22, 2021.
Hafla ya kuapishwa kwa Wakuu hao wa Wilaya imefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Brig. Jen. Wilbert Ibuge.
Jumla ya Wakuu wa Wilaya watano (5) wameteuliwa hivi karibuni kuongoza Wilaya 5 za Mkoa wa Ruvuma ambazo ni Songea, Namtumbo, Mbinga, Nyasa na Tunduru ambapo kati yao wawili ni teuzi mpya, wawili wakiendelea kubaki kwenye Wilaya zao za awali na mmoja akihamia kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala
Wakuu wa Wilaya walioteuliwa kwa mara ya kwanza ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Col. L. R Thomas na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Julius Keneth Ningu, huku Wakuu wa Wilaya ambao wanaendelea na nyadhifa zao ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Amina Ally Mangosongo ambaye ametokea Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara.
Wengine walioteuliwa kuendelea na nafasi zao ni Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Polotet Kamando Mgema na Mhe. Julius Mtatiro ambaye anaendelea kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.
Na Salum Said,
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Juni 22, 2021
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit