Na Silvia Ernest
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Mbinga Inspekta John Lupondije ametembelea na kukagua miundombinu ya kizimamoto katika ujenzi unaoendelea kutekelezwa Shule za msingi Ilela, Nyoni pamoja na Shule mpya ya msingi inayojengwa katika Kata ya Kipapa.
Inspekta Lupondije amebainisha kuwa lengo la kutembelea utekelezaji huo ni kukagua miundombinu ya kizimamoto katika miradi inayotekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga hususan katika ujenzi wa shule.
Aidha ametoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuendelea kuzingatia miundombinu ya kizimamoto wakati wa utekelezaji wa miradi.
"Tuendelee kuzingatia miundombinu ya kizimamoto katika miradi tunayotekelezwa ili kuepusha hasara zinazoweza kutokea endapo miundombinu hiyo itakosekana" Amesisitiza Lupondije
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit