Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango (FUM) imefaanya ziara ya kumetembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga tarehe 06 Mei 2024.
Katika ziara hiyo kamati imetembelea ujenzi wa nyumba 3 za Wakuu wa idara ambazo zinagharimu Tshs. 360,274,650, ambapo kiasi cha Tshs. 240,000,000 fedha kutoka Serikali Kuu na Tshs. 120,274,650 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.
Vilevile kamati imekagua ujenzi wa wodi 3 za kulaza wagonjwa ( wanawake, watoto na wanaume) zinazojengwa katika hospitali ya Halmashauri ambapo ujenzi huo utagharimu kiasi cha Tshs.500,000,000.
Aidha kamati imetembelea ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Hagati ambao utagharimu kiasi cha Tsh. 128,000,000 pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana Shule ya Msingi Maguu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Imeandikwa na Silvia Ernest
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tarehe 07 Mei 2024
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit