Na Silvia Ernest
Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma imeridhishwa na utekelezeaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Imemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuongeza kasi katika utekelezaji huo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa Oktoba 10, 2023 na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Ndg. Mohamed Ally katika ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
" Tumetembelea miradi na tumeona utekelezaji wake, Mkurugenzi endeleza ari hiyo ili miradi hii itekelezwe katika ubora na viwango tarajiwa" Amesema Ndg. Ally
Pamoja na pongezi hizo amewashukuru wananchi wa Kata ya Kipapa kwa kuona haja na kutoa eneo lenye ukubwa wa ekari 5 na nusu kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Msingi Kilango.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga Mhe. Joseph Mdaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
" Kipekee sana nimshukuru Mhe. Rais wetu kwa kutuona wana Mbinga na kutuletea fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi hii tunashukuru sana" Amebainisha
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit