Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amewataka wananchi wa Kata ya Kipapa kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuimarisha ulinzi wa vifaa vya ujenzi pamoja na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa katika ubora na viwango vinavyohitajika.
"Ni wajibu wa kila Mtanzania kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuna wengine wanaiba vifaa vya ujenzi tunajikomoa sisi wenyewe na sio watu wengine tusimamie miradi kwa pamoja tusiwaachie wataalam pekee yao" Amebainisha Kanal Laban
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo 4 Julai 2023 katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi inayojengwa katika Kata ya Kipapa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 9 , ujenzi wa matundu ya vyoo 18 pamoja na ujenzi wa jengo la Utawala, ujenzi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa BOOST.
Pamoja na rai hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amemshauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kutowapa kazi ya ujenzi mafundi wenyeji ambao sio waminifu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuona fedha inayotolewa inaendana na utekelezaji wa miradi.
" Mkurugenzi usimpe mradi fundi ambae hatekelezi vizuri miradi, Serikali ilileta utaratibu mzuri sana wa kujenga kwa kutumia mafundi wenyeji tulionao katika maeneo yetu lakini kuna baadhi ya mafundi hao sio waaminifu wanaharibu miradi
Hatuwezi kukubali kwasababu tu ni kijana wa maeneo yetu basi atuharibie miradi yetu miradi inaharibiwa kwa sababu tu tunahafamiana" Amesisitiza Kanal Laban
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amemhakikishia Mhe. Mkuu wa Mkoa kuwa maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili utekelezaji wa ujenzi huo ukamilike kwa wakati na katika ubora.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit