Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani (International Women's Day) ambayo kwa Mkoa wa Ruvuma yamefanyika leo Machi 8 katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba iliyopo Wilayani Songea Mgeni Rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa huo Brig. Jen. Balozi Wilbert Ibuge.
Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Halmashauri wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Mwanaidi Mang’uro, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Desderius Haule, Mkurugenzi Mtendaji Juma Haji, Wakuu wa Idara, Vitengo na watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na wale kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbinga wameungana na wenzao kutoka Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma katika siku hii muhimu ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu imefanyika ikiwa na Kauli Mbiu isemayo "KIZAZI CHA HAKI NA USAWA KWA MAENDELEO ENDELEVU; TUJITOKEZE KUHESABIWA"
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit