Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Aziza Mangosongo ameongoza Kamati ya Sherehe ya Wilaya kwenye kikao cha maandalizi ya ujio wa Mwenge wa Uhuru Wilayani Mbinga, kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Oddo Mwisho uliopo Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Kikao hicho kimelenga kujadili maandalizi ya ujio wa Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2021, vilevile kimefanya tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizopita ambazo zilizofanyika mwaka 2019.
Kupitia kikao hicho kamati mbalimbali za maandalizi zimeundwa kuelekea ujio huo wa Mwenge wa Uhuru ambazo ni Kamati ya Chakula na Vinywaji, Fedha na Mipango, Kamati ya Mapokezi na Malazi, Ujenzi na Mapambo na Kamati ya Usafiri na Usafirishaji.
Kamati nyingine ni Afya na Maji, Ulinzi na Usalama, Kamati ya Miradi, Risala na Ratiba, Uhamasishaji, Kamati ya Zawadi na Sare pamoja na Kamati ya Uhamasishaji.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2921 wilayani Mbinga unatarajia kukagua, kutembelea, kuweka mawe ya msingi na kufungua jumla ya miradi 10 ya maendeleo, ukiwa na ujumbe unaosema TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU, ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI.
Kamati hiyo ya Sherehe ya Wilaya, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Mangosongo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga inatarajia kukutana tena Agosti 5 kupitia maandalizi, miradi na utendaji kazi wa kamati mbalimbali za maandalizi zilizoundwa.
Imeandikwa na
Salum Said
Afisa Habari, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Julai 22, 2021
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit