Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeongoza kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2021/2022 mara baada ya kufanyika kwa tathimini ya utekelezaji wa Mkataba huo ngazi ya Mkoa Halmashauri hiyo imeibuka kinara kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma
Akizungumza wakati wa Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Robo ya Pili kilichofanyika Machi 3 kwenye Ukumbi Shule ya Sekondari Kiamili, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imefanya vizuri kwa kutelekeza kwa ukamilifu afua zote za lishe kwa mujibu wa mkataba kwa vipindi viwili mfululizo vya utekelezaji wa Mkataba huo kwa mwaka huu wa fedha kuanzia Julai hadi Desemba 2021/2022
Mhe. Mangosongo amewapongeza watumishi na watendaji wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga pamoja na wadau wote wa lishe kwa kufanya vizuri katika utelekezaji wa mkataba na kutoa wito wa kuendelea kushirikiana na kuhakikisha suala la lishe linapewa kipaumbele na kuwa ajenda ya kudumu kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi ngazi ya wilaya na kupongeza uongozi wa Halmashauri kwa kuanzisha Klabu za Lishe kwenye shule ili kuongeza ufahamu na uelewa wa suala la lishe kwa wanafunzi.
Naye Bi. Janeth Bandari ambaye ni Afisa Lishe, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga amewashukuru wadau wote kwa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha suala la lishe linakua mtambuka kuanzia ngazi ya kaya na kijiji huku akizitaja kata tatu za Lukarasi, Wikiro na Amanimakolo kuwa ndizo zilizofanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa mkataba wa lishe miongoni mwa kata 29 za Halmashauri ya hiyo kwa kipindi cha robo ya pili.
Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kiliambatana na upimaji wa hali ya lishe kwa wajumbe wote wa kikao lililohusisha kufanyika kwa tathimini ya uwiano kati ya uzito na urefu, zoezi ambalo liliongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mbinga ambaye pia alikua Mwenyekiti wa kikao hicho.
Imeandikwa na
Salum Said, Mbinga
Tarehe 3 Machi, 2022
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit