MBINGA DC KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MASHIRIKI YA KIDINI KATIKA SEKTA YA AFYA
Na Silvia Ernest
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga itaendelea kushirikiana na mashirika ya kidini katika kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya hususan huduma ya mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 5 Julai 2024 na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura katika kikao cha tathmini ya makubaliano ya utoaji wa huduma za afya baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Jimbo Katoliki la Mbinga kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2023.
Mkurugenzi Kashushura amebainisha kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa mashirika ya kidini katika kutoa huduma bora za afya nchini.
“Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na mashirika ya kidini ni ahidi kwamba ushirikiano huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga utakuwa endelevu”
Kwa upande wake Askofu wa Jimbo la Mbinga John Ndimbo amemuomba Mkurugenzi Kashushura kusaidia kutatua changamoto ya upungufu wa watoa huduma za afya katika Hospitali ya Litembo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ili hospitali hiyo iendelee kutoa huduma bora na kuwafikia wananachi wengi zaidi.
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kutoa taarifa pindi wanapogundua wafanyabiashara ambao wanakiuka taratibu hatua ambayo itapelekea kudhibiti upotevu wa mapato.
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit