• Wasilina nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mbinga District Council
Mbinga District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • HISTORIA
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Afya
      • Elimu
        • Msingi
        • Sekondari
      • Maji
      • Community Development
      • Menejimenti ya Mipango na Takwimu
      • Mifugo
      • Agriculture,Cooperative and Irrigation
      • Utawala
      • Fedha na Biashara
    • Kitengo
      • Habari, mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Investment
    • Makaa Ya Mawe
  • Huduma
    • Huduma za afya
    • Huduma za Elimu
  • Councillors/PM
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • UKURASA WA ELIMU SEKONDARI
    • Mbunge
      • Miradi iliyo inayofadhiliwa
      • Ratiba ya Mbunge
      • Ligi ya Mbunge
  • Miradi
    • Miradi
      • Miradi Mipya
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi ambayo haijakamilika
  • Chapisho
    • Miongozo
      • TEHAMA
    • Kanuni
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • TEHAMA
    • Idara
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Tarafa
    • Mbuji
      • KARIBUBU KATA YA MBUJI
      • Litembo
      • Kitura
      • Nyoni
      • Mpapa
      • Kata ya Kilangajuu
      • Maguu
      • Langiro
    • Kigonsera
      • Kigonsera
      • Kihangimahuka
      • Kitumbalomo
      • Matiri
    • Hagati
    • Mkumbi
    • Namswea
    • Mkumbi
      • Mkumbi
      • Kipololo
      • Ukata
      • Ngima
  • MIFUMO

MBINGA DC NA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UGONJWA WA USUBI

Tarehe ya kuwekwa: September 15th, 2023

Na Silvia Ernest, Mbinga DC


Katika kuhakikisha  kuwa Halmashauri ya Wilaya ya mbinga inatokomeza  kabisa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hususan Usubi, Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeendelea kuongeza nguvu  kila mwaka katika kampeni ya  umezaji  wa dawa kinga za Usubi  kwa wananchi wanaoishi  katika kata 29  za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.


Kauli hiyo inathibitishwa kitakwimu na ongezeko la  idadi ya wananchi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambao wamejitokeza kumeza dawa za kinga tiba za Usubi mwaka 2023 ukilinganisha na mwaka uliopita yaani 2022.


Katika mwaka 2022  Halmashauri ilijiwekea lengo la kuwafikia wananchi 283, 531 na wananchi waliofikiwa ni 237, 249 sawa na 84% , kwa mwaka huu  2023  lengo lilikuwa kuwafikia wananchi  228,466   na wananchi 229, 414  walifikiwa  ndani ya siku saba sawa na 100. 4%.


Takwimu hizo zinaonesha  dhahiri kuwa jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia  Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga zinazaa matunda katika kuhakikisha ugonjwa huu wa Usubi na magonjwa mengineyo yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yanatomezwa.


Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Halmashauri  ya Wilaya ya Mbinga Dkt. Amad Mwalukunga alibainisha kuwa baada ya kubaini muitikio mdogo wa wananchi wa kumeza dawa za Kinga tiba za usubi kwa mwaka uliopita Halmashauri ilijiwekea  mikakati ya kutatua changamoto hiyo.


Moja ya mkakati uliowekwa wa kuwafikia wananchi ni kufanya Mkutano na wananchi na kutoa elimu juu ya ugonjwa huo ili wananchi wapate uelewa wa kutosha wa dalili, madhara, kinga na tiba  ya ugonjwa wa Usubi kabla ya kumeza dawa hizo.


Pili ni  kuhakikisha  wataalam waliopewa mafunzo kitaalam  kutoka katika ngazi ya jamii  wanapita    kila Kaya/ nyumba  kutoa   dawa za Kinga tiba za Usubi ili kumfikia kila mwananchi na kuepusha usumbufu na gharama kwa wananchi kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya kumeza dawa hizo.


" Serikali iliona ni ngumu sana  kwa wananchi kuja katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya na kupata hizi dawa kwahiyo mkakati tuliokuja nao ni kupita katika kila nyumba ili kuwafikia wananchi wote" Alisema Dkt. Mwalukunga


Aliongeza " Kabla ya kuwapatia dawa hizo tulitoa elimu ya kutosha  ili kuondoa dhana potofu zinazosemwa na wanajamii  kuhusu hizi dawa na kuwaelewesha wananchi juu ya madhara yanayoweza kupatikana kama hujameza dawa hizi"


Mwalukunga

alihitimisha  kuwa mategemeo ya Halmashauri kwa mwaka ujao  2024 ni kuhakikisha kila mwananchi  ambaye ana umri wa miaka kuanzia mitano ambae sio mjamzito au mgonjwa mahututi anafikiwa na zoezi la umezaji wa dawa za Kinga tiba za Usubi.


Mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt.Joseph Washa Washa  alibainisha kuwa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele   hapo awali ni pamoja  ugonjwa wa Usubi,  Minyoo ya tumbo ,Kichocho , Matende na Mabusha pamoja na Trakoma.


Alieleza kuwa uelewa wa wananchi  juu ya dalili, madhara pamoja na kinga  ya magonjwa haya ni mdogo sana na pale mwananchi anapofika kugundua dalili tayari ugonjwa umeshaleta madhara makubwa.


" Kuna wananchi ambao wana ugonjwa wa usubi lakini  hawajui  kama wanao  kwahiyo ni mhimu sana kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili sasa waelewe,   na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga tunafanya hilo" Alisema Washawasha


Akizitaja dalili za ugonjwa wa Usubi ni  ngozi kuwasha, ngozi kuwa  na mabakamabaka kama ya kenge, uoni hafifu  pamoja na upofu.


Bila kukwepesha Washa washa alibainisha  kuwa madhara  ya ugonjwa ya Usubi ni  makubwa ikiwemo kuleta  upofu, ngozi kuwa na madoa madoa kama ya chui pamoja  kupoteza nguvu kazi katika shughuli za kiuchumi pindi mwananchi anapopata madhara tajwa.


 Amethibitisha kuwa kinga na tiba za ugonjwa wa Usubi zipo, mwananchi anatakiwa  kumeza dawa za kinga tiba ai…

Matangazo

  • TANGAZO LA KAZI September 17, 2024
  • TANGAZO LA HESABU MBINGA DC July 01, 2024
  • TANGAZO LA KAZI YA MKATABA NAFASI YA MKUSANYA USHURU January 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA YA MKATABA- DEREVA NAFASI 2 January 25, 2024
  • Tazama zote/kote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI KASHUSHURA ATOA MSISITIZO MATUMIZI YA NISHATI SAFI SHULENI

    February 15, 2025
  • MAAFISA TUME WATEMBELEA MBINGA DC

    January 08, 2025
  • WAANDISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA ANGALIZO

    January 09, 2025
  • KASHUSHURA AWAPONGEZA WANANCHI UJENZI WA SHULE

    September 10, 2024
  • Tazama zote/kote

Video

UGAWAJI WA MKAA MBADALA
Video zaidi

Kurasa za haraka

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Utumishi
  • Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
  • Tovuti ya Ikulu
  • Jeshi la Polisi Tanzania
  • Mamraka ya mapato Tanzania (TRA)

Waliotembelea tovuti

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ili kutufikia

Wasilina nasi

    MBINGA DISTRICT COUNCIL

    Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA

    Namba za simu: 2552640005

    SImu ya mkononi: PS 0754533018

    parua pepe: ded@mbingadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit