Na Silvia Ernest
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeendelea kutekeleza agizo la kampeni ya Kitaifa juu ya upandaji wa miti 1, 500,000 kwa mwaka kwa kila Wilaya nchini.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Mazingira Bw. Chrispine Haonga amebainisha kuwa pamoja na jitihada za uhifadhi wa Mazingira, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imeotesha miche ya miti mbalimbali katika kitalu cha miti cha Mpapa kwa ajili ya matunda,mbao,dawa pamoja na vyanzo vya Maji
Akielezea baadhi miche iliyopo, Haonga amesema kuna miche ya Msindano, Msederela ambao hutumika kwa mbao, Myenda ambao ni chanzo cha maji na mbao, Mbatabata ambao ni dawa, Mzambarau,Msambia na Karanga laini wenye faida ya matunda.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kupanda miti katika maeneo yao ili kunufaika na miti hiyo hususani katika kutunza mazingira pamoja na kukuza uchumi.
Mwisho ametoa wito kwa wananchi wote kuilinda misitu na uoto asili dhidi ya moto na uanzishaji holela wa shughuli za kibinadamu.
Amesema "Serikali inasisitiza katika upandaji miti katika maeneo yetu, hii ni faida kubwa sana katika Halmashauri yetu tutapata faida ya dawa, matunda lakini pia itasaidia katika kukuza uchumi wetu hasa katika miti ya mbao"
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit