Kamati ya Sherehe ya Wilaya ya Mbinga chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Aziza Mangosongo imekutana na kufanya kikao cha maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu 2023.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kigonsera ikiwa ni hatua muhimu katika kufanya maandalizi ya msingi na ya awali kuhusiana na ujio wa Mwenge huo wa Uhuru kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kukutanisha wadau mbalimbali wa Mwenge wakiwemo viongozi wa serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, watumishi wa sekta na taasisi mbalimbali za umma na binafsi pamoja na madiwani.
Kupitia kikao hicho wajumbe walianza kwa kufanya tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Mbinga hususani Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mwaka uliopita wa 2022 kabla ya kujielekeza kujadili na kuweka mipango na mikakati ya kuupokea Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu unatarajiwa kuwashwa Mkoani Mtwara mapema mwezi Aprili.
Katika hatua nyingine Mhe. Mangosomo ameelekeza Halmashauri kupitia Mkurukugenzi Mtendaji na Menejimenti yake kuanza haraka mchakato wa kuainisha miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2023 sambamba na mapendekezo ya njia (route) ya Mwenge.
Vilevile kupitia kikao hicho Mkuu wa Wilaya ametoa wito wa kuanza kufanyia kazi uundwaji wa Kamati mbalimbali za Mwenge unakaotakiwa kwenda sambamba kuhuisha wajumbe wa kamati hizo na uteuzi wa wajumbe wapya pale itakapohitajika kufanya hivyo.
Ratiba ya awali ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2023 inabainisha kuwa Mwenge huo utawashwa Mkoani Mtwara mwanzoni mwa mwezi Aprili ambapo unatarajiwa kupokelewa Mkoani Ruvuma kupitia Wilaya ya Tunduru tarehe 17 Aprili na hatimaye kuingia na kukimbizwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Aprili 22
Imeandikwa na Salum Said
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Tarehe 16 Februari, 2023
MBINGA DISTRICT COUNCIL
Sanduku la posta: P.O. BOX 194 MBINGA-RUVUMA
Namba za simu: 2552640005
SImu ya mkononi: PS 0754533018
parua pepe: ded@mbingadc.go.tz
Copyright ©2021 Mbinga District Council. All rights Reserved. Prepared by ICT - Unit